MSANII mkali wa kuchekesha na sanaa za jukwaani Afrika Mashariki, Anne Kansiime anatarajiwa kufanya onyesho lake Agosti 2, mwaka huu katika Ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo linaloandaliwa na kituo cha Redio 5 litaambatana na burudani ya muziki kutoka kwa Odama Band, pamoja na mchekeshaji Fredi Omondi kutoka Kenya na Pilipili wa Tanzania.
Akizungumzia onyesho hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Redio 5, Robert Francis alisema wameamua kumualika Kansiime kwa sababu ana kipaji cha hali ya juu katika uchekeshaji na ana mashabiki wengi Tanzania.
“Kansiime ni mchekeshaji ambaye amejizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki kwa uwezo wake wa kuweka utani kwenye maisha ya kawaida,” alisema Francis.
Cheki Moja ya Comedy Zake Hapo chini
Kansiime maarufu katika mitandao ya kijamii, alianza kwa kuweka vipande vya video akiigiza kama mwanamke wa Kiafrika anayekutana na changamoto mbalimbali za maisha.
Pia, huendesha kipindi cha ‘Don’t Mess With Kansiime’ kwenye kituo cha Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye kipaji cha pekee nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla. Onyesho hilo la Kansiime, limepewa jina la Cheka Kwa Nguvu, na tiketi zitauzwa Sh.90,000 kwa mtu mmoja na Sh.700,000 kwa meza ya watu wanane.

0 comments :

Post a Comment

 
Top
Bongohots.blospot.Com