
Abiria wote wa ndege ya Air Algerie waliangamia jangwani
Abiria wote na wahudumu wa ndege ya Air Algerie AH5017 waliangamia jangwani.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametangaza
kuwa majeshi ya ufaransa yamefaulu kupata mabaki ya ndege lakini
hawakuweza kuokoa nafsi hata moja.
Aidha rais Francois Hollande ametangaza kuwa
majeshi hao wamepata mtambo wa kunukuu sauti ''Blackbox'' huko Mali
ilikoanguka ndege hiyo iliyokuwa ikielekea mji mkuu wa Algeria Algiers.

Abiria wote wa ndege ya Air Algerie waliangamia jangwani
Ndege hiyo ilikuwa imetoka mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou ikiwa na Abiria 110 na wahudumu 6 .
Abiria 51 waliokuwa ndani ya ndege hii walikuwa ni raiya wa Ufaransa.
Wengine walikuwa 27kutoka Burkina Faso, 8
kutoka Lebanon , 6 kutoka Algeria , 2 kutoka Luxembourg, 5 kutoka
Canada, Wajerumani 4 .

Jamaa ya wahasiriwa wanakutana huko Ougadougu Burkina Faso
Abiria wengine walikuwa mmoja kutoka mataifa ya Cameroon , Ubeljiji ,Misri Ukraine Uswisi Mnigeria na mmoja kutoka Mali.
Waziri wa Usalama wa ndani wa Ufaransa Bernard
Cazeneuve alisema ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Algiers kutoka mji
mkuu wa Burkina Faso , Ougadougou,ilianguka kutokana na hali mbaya ya
anga
0 comments :
Post a Comment