Al-Shabaab imekuwa ilkilazimisha kutorosha watoto
kutoka katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wao kwa kisingizio kwamba
wanatoa malazi na elimu kwa vijana wasio na makaazi na wasiotunzwa,
wazazi wanaohusika na wazee waliiambia Sabahi.
Lengo la kituo hiki ni kurekebisha watoto "wasiotunzwa" na kuwapa
elimu ya dini, kiongozi wa al-Shabaab katika Shabelle ya Chini Sheikh
Mohamed Abu Abdalla alisema katika ujumbe wa sauti uliotumwa katika
tovuti ya Redio Al-Furqaan, msemaji kwa niaba ya kikundi.
"Ni kituo cha kurekebisha watoto ambao wamepotoka au wasio na makaazi
na ambao wameachwa bila kutunzwa na umma," Abdalla alisema katika
uzinduzi.
Zaidi ya mayatima, alisema, kituo kitawapokea watoto wengine ambao
wanahitaji kurekebishwa na kutoa wito kwa wazazi wa watoto walioacha
shule na familia zinazorejea Somalia kutoka nje ya nchi kuandikisha
watoto wao.
"Watoto waliorudi Mogadishu wakitokea nchi za Magharibi wanahitaji
urekebishaji," alisema. "Ninatoa wito kwa watu waliotawanyika duniani
wakitokea Somalia kutumia fursa hii [ya kituo hiki]."
Lakini licha ya kuhudumia watoto mayatima na walio katika mazingira
hatarishi, kituo hiki kimejazwa watoto waliochukuliwa majumbani kwao na
shuleni, alisema Sultan Ali Hassan Ibrahim, mzee mwenye umri wa miaka
60-kutoka Barawe ambaye alikimbilia Mogadishu mnamo Novemba 2013
kutokana na wasiwasi juu ya usalama wake.
"Watu [wa Barawe] hawako huru,
kwa hiyo watoto wao wanawekwa katika makambi yanayoitwa ya urekebishaji
pasipo ridhaa yao," aliiambia Sabahi. "Wamewaweka vijana wadogo katika
makambi, hususani watoto wa kati ya umri wa miaka 12 na 16, ambao
wanaamini wanaweza kuwatia kasumba kwa haraka kuamini kile
wanachoridhishwa."
Ibrahim alisema al-Shabaab imefungua makambi yanayofanana na hayo ya
kutia kasumba huko Sablale katika Shabelle ya chini, na huko Buale, mji
mkuu wa Jubba ya kati.
Alisema watoto sita ambao alikuwa na uhusiano nao ni miongoni mwa hao waliotoroshwa na al-Shabaab.
"Hawatenganishi watoto. Hata hivyo wamekuwa wakiwachukua wale
wanaokwenda shule na wale wanaojifunza katika misikiti," alisema.
"Watoto hawaruhusiwi kutembelewa na ndugu zao."
Hila za kuongeza tena wapiganaji wa al-Shabaab
Pamoja na madai ya al-Shabaab, lengo la kundi la wanamgambo ni
kuongeza tena vyeo vya wapiganaji ambavyo walipoteza katika mapigano,
alisema Mohamed Yaqub, mwenye umri wa miaka 38, ambaye alikimbia kutoka
Barawe pamoja na mke wake na watoto wakati al-Shabaab walipoteka eneo
hilo.
"Wanataka kuwaingiza katika jeshi watoto na kuwatumika katika mapigano," alisema. "Kusudi lao sio kuwahudumia [kama walivyodai]."
Abukar Sheikh Hassan, mzee wa mila mwenye umri wa miaka 55 ambaye pia
alikimbia kutoka Barawe miaka miwili iliyopita ambaye sasa anaishi
Mogadishu, aliiambia Sabahi kwamba wananchi wa Barawe wana wasiwasi wa
siku zijazo za watoto wao.
"Kusudi la al-Shabaab sio kuwafundisha watoto Qur'an na dini, bali wanataka watoto kujilipua wenyewe," aliiambia Sabahi.
Hassan alionyesha wasiwasi wake kwamba watoto wanaweza kurejea
nyumbani kuua familia zao na wananchi wenzao wa Barawe ambao
walibadilishwa mawazo na mtazamo uliobadilika na vurugu za al-Shabaab.
"Watu ambao wangekuwa sehemu katika maendeleo ya mkoa kwa kupata
elimu nzuri na kuusaidia umma wanakuwa watu ambao wanapita njia
isiyofaa," alisema.
Kutangaza kufunguliwa kwa Kituo cha al-Amal, al-Shabaab walituma
picha za watoto waliovaa sare safi na wakiwa wameshikilia nakala za
Qur'an, wakidai kwamba maisha ya watoto hao yamekuwa bora zaidi.
Lakini Hassan alisema kwamba ni propaganda tu ambazo al-Shabaab
wanatumia kuwatega watoto na kuwashawishi wazazi kuja katika maeneo
yaliyopo chini ya udhibiti wa al-Shabaab kwa ajili ya kutafuta maisha
mazuri.
Badala yake, alisema serikali ya Somalia inapaswa kutoa huduma za
kuboresha maisha ya watoto wasiokuwa na makazi na yatima ambao hawana
mtu kuwatunza.
"Serikali inapaswa kukamilisha wajibu wake na kuonyesha utawala bora
na kuwatunza watoto," alisema. "Vinginevyo al-Shabaab watachukua wajibu
huo na kuwabadilisha mawazo watoto.
0 comments :
Post a Comment