
Marehemu Henry Lyimo enzi za Uhai wake
Kwa mujibu wa habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba Mwandishi wa habari na Mtangazaji maarufu wa kipindi cha Michezo cha redio Moshi FM ya mkoani Kilimanjaro Henry Lymo maarufu pia kwa jina la Kipese amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Meneja wa Vipindi Redio Moshi FM Yusuph Mazimu amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Kilema, Marangu Moshi.
Marehemu Henry Lymo mwenye tisheti nyekundu enzi za uhai wake akihojiwa na Mtangazaji wa sasa wa Kahama Fm Halid Mchopa
Inasemekana Kipese amepata ajali ya pikipiki kwa kugogwa na gari wakati akitoka kuchezesha mechi ya mpira wa miguu maeneo ya himo mkoani Kilimanjaro.


0 comments :
Post a Comment