Jeshi la Israel jana lilishambulia mji wa Gaza kwa makombora yenye uzito na kufanikiwa kuharibu alama muhimu ya utawala wa kikundi cha Hamas.

Shambulizi hilo lilisababisha vifo vya wapalestina 128 na  kusababisha zaidi ya mamilion ya watu kukosa umeme baada ya mitambo ya umeme kuharibiwa vibaya katika mashambulizi hayo yaliyofanywa siku ya jumanne.

Kwa mujibu wa afisa wa afya wa Palestina Ashraf al Kidra alipozungumza na Associated Press alisema vifo vya jana vinatimiza idadi ya wapelestina waliokufa kutokana na vita hivyo kufikia 1,229 huku zaidi ya 7,000 wakibaki na majeraha, ilihali serikali ya Israel ilisema imepoteza uhai wa wanajeshi wake 53.

Pamoja na madhara yanayoendelea kutokea baina ya nchi hizo mbili, pande zote mbili zinasisitiza kutositisha mashambulizi.

Kiongozi wa Hamas alisema hawatasitisha mashambulizi ya roketi mpaka pale watakapotimiziwa matakwa yao, huku waziri mkuu wa Israel naye akiwaonya waisrael kujiandaa kwa vita zaidi
Hata hivyo jitihada za kimataifa zinazoongozwa na Misri zinaendelea ili kusitisha mapigano hayo kwasababu za kubinadamu.

0 comments :

Post a Comment

 
Top
Bongohots.blospot.Com