MISS Tanzania
2006/07 Wema Sepetu amesema ugonjwa wa ngozi ulioshambulia sehemu ya
shavu lake la kushoto umeharibu urembo wake na kumfanya ashindwe kutoka.
Miss Tanzania 2006/07 Wema Sepetu.
Akizungumza
kwa huzuni na Zee la Udaku, Wema alisema hakutegemea kama tatizo hilo
lingekuwa kubwa, kwani lilianza kama kipele kidogo ambacho baadaye
sehemu kubwa ilivimba na kuharibu mwonekano wake.
“Ulianza muwasho, kikawa kipele kisha kikageuka kama kishilingi.
Nilipokwenda
hospitali nilipewa dawa ya crime ya kupaka, mimi nikachua eneo
lililoathirika, kumbe ndiyo nikawa nasababisha matatizo, kukavimba zaidi
kama unavyoona,” alisema Wema ambaye alikataa kupigwa picha.

0 comments :
Post a Comment