Maisha
ya kimapenzi kila ikiitwa leo yanazidi kubadilika ujuzi uliokuwa nao
jana yawezekana wazi kabisa leo sio ujuzi kabisa ila ni kitu cha kawaida
kwa baadhi ya watu sasa chukua mda mfupi kusoma makala hii utajifunza
kitu MMMH mshaanza eti nimeisha ingia mama Chaunabe kitanga na njia
nisiye na bleki kwenye domo langu, wahenga wanasema kinywa cha mkubwa
kinanuka lakini maneno hayanuki. Najua maneno yangu ya shombo huenda
hayakufurahishi wewe ambaye kila kukicha unabadili wanaume na kuonekana
una
hila.
Shutuuu dada mwanamke tabia babu wee, mwanamke kujua mumeo anataka
nini, mwanamke kujituma kwenye kiwanja kifupi cha sita kwa sita.
Unasahau cha kumvutia mwanaume unakimbilia kuukoboa mwili nani kakuambia
weupe mali? Basi mkaa usinge nununuliwa! Tena leo nakazi na wewe,
nani kakuambia weusi ni laana. Basi leo nataka nikuambie wewe usiye na
haya uliyemaliza vipodozi mwisho wa siku uso unakuparama kama mchawi
mzee, unalo hilo? Siri ya weusi maana yake ni utamu hata zambarau tamu
ni nyeusi, zabibu tamu ni nyeusi na hata usingizi mtamu unapatikana
usiku mweusi. Huoni Mzungu akimuonja mswahili
anachanganyikiwa.
Wewe unajikoboa Mzungu ajipake masizi? Acha ubwege. Nimejikuta hata
nikisahau kuelezea nilichokikusudia kwa ajili ya malimbukeni wachache,
jivunie weusi wako babu wewe. Tuachane na hayo ambayo kwa kiasi
nimejikuta nikipandwa na mzuka na kuingia kwenye mada nyingine. Kama
unabisha mwangalie jirani yako anayetumia mkorogo ngozi kama kuku wa
mayai aliyezeeka.
0 comments :
Post a Comment