Robo fainali ya tatu ya michuano ya mataifa ya Ulaya 2016 imechezwa usiku wa July 2 2016 kwa kuzikutanisha timu za taifa za Ujerumani dhidi ya timu ya taifa ya Italia, huu ni mchezo ambao mashabiki wa soka kwa kiasi kikubwa walikuwa wanautabiria ndio mchezo utakaotoa Bingwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2016.
4764
Rekodi za timu hizo mbili zilikuwa zinaonekana kuwa nzuri kwa Italia kuliko Ujerumani, kitu ambacho hakikuisaidia Italia kupata matokeo, kabla ya mchezo wa leo Italia alikuwa kamfunga Ujerumani mara 15 katika michezo 34 waliowahi kucheza, sare mara 11 na kupoteza mara 8, bahati ilionekana kutokuwa nzuri kwa Italia baada ya kukubali kipigo cha mikwaju ya penati 6-5.
4253
Hatua ya mikwaju ya penati ilikuja baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya goli 1-1, magoli ambayo yalifungwa na mesut ozil kwa Ujerumani dakika ya 65, lakini Italiawalikuja kuchomoa goli hilo dakika ya 78 kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Leonardo Bonucci. Kwa matokeo hayo Ujerumani itakutana na mshindi kati ya Ufaransa naIceland katika hatua ya nusu fainali.

2 comments :

 
Top
Bongohots.blospot.Com