Odion Ighalo
Mshambuliaji wa Manchester United Odion Ighalo, 30, amepigwa marufuku katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo kutokana na hofu ya hatari ya maambukizi ya virusi vya corona.
Ighalo ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya United kutoka klabu ya Shanghai Shenhua hadi mwisho wa msimu amekuwa akifanya mazoezi na mkufunzi wa kibinafsi katika eneo tofauti mjini Manchester.
Mshambuliaji huyo alitakiwa kufanya mazoezi mbali na uwanja wa mazoezi wa Man United kutokana na maswala ya usalama wa kiafya kutokana na mlipuko wa virusi vya corona nchini China ambao umewaua zaidi ya watu 1100.(Mirror)
Liverpool inapanga kumnunua mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, 23, mwisho wa msimu huu huku dau la £46m likitosha kumsaini . (Bild)
Mshambuliaji wa Barcelona Philippe Coutinho, 27, amekataa uwezekano wa kurudi katika klabu ya Liverpool akidai kwamba yuko katika safari. (Sun)

Phillipe Coutinho










































































































































Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

0 comments :

Post a Comment

 
Top
Bongohots.blospot.Com