
WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Erikisongo wilayani Monduli wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni yao kuteketea na moto leo asubuhi.
Moto
huo ambao inaelezwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme ulizuka wakati
wanafunzi hao wakiwa darasani. Hakuna mtu yoyote aliyedhurika lakini
mali kadhaa za wanafunzi zimeteketea.
Kikosi
cha Zimamoto kutoka Arusha kilifika wakati tayari mabweni hayo
yameshateketea. Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa ametembelea shule
hiyo na kuahidi kuwasafirisha wanafunzi majumbani kwao wakati utaratibu
unafanywa kurejesha mabweni hayo katika hali ya kawaida.


0 comments :
Post a Comment