Meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho, amekiri kufurahishwa na uwezo wa beki wa kushoto kutoka nchini Brazil Filipe Luis, wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Wolfsberger AC ya nchini Austria uliochezwa usiku wa kumakia hii leo.
Mourinho, amesema beki huyo ambaye alimsajili majuma mawili yaliyopita akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Hispania Atlertico Madrid, ameonyesha kiwango cha hali ya juu.
Amesema alidhani Filipe huenda angecheza chini ya kiwango kutokana na muda mfupi alioupata wa kufanya mazozi na kikosi cha Chelsea tangu alipowasili jijini London, lakini imekuwa tofauti.
Meneja huyo kutoka nchini Ureno amesema kutokana na hali aliyoiona kwa beki huyo wakati wa mchezo dhidi ya Wolfsberger AC ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao moja kwa moja, anatarajia mazuri kutoka kwake katika kipindi chote cha msimu.
Mourinho, pia akatoa pongezi kwa wachezaji makinda aliowatumia katika mchezo huo, kwa kusema walicheza vizuri na kuchangia upatikanaji wa bao la kusawazisha baada ya Chelsea kuwa nyuma kwa dakika 28.
Bao la kusawaisha la Chelsea lilifungwa na Jeremie Boga katika dakika ya 83 huku bao la wenyeji likipachi na Silvio Carlos katika dakika ya 55

0 comments :

Post a Comment

 
Top
Bongohots.blospot.Com