Nembo ya Timu ya Simba
Posted Jumatatu,Julai28 2014 saa 14:34 PM
In Summary
Usajili huo unaingia katika rekodi kwani umemnasa
mchezaji wa hadhi kubwa lakini kwa dau la Sh5 milioni tu. Katika hali ya
kawaida, mchezaji mwenye hadhi ya Kisiga husajiliwa kwa kati ya Sh10
milioni hadi 30 mil
Usajili huo unaingia katika rekodi kwani umemnasa
mchezaji wa hadhi kubwa lakini kwa dau la Sh5 milioni tu. Katika hali ya
kawaida, mchezaji mwenye hadhi ya Kisiga husajiliwa kwa kati ya Sh10
milioni hadi 30 milioni.
Akizungumza na Mwanaspoti baada ya kusaini mkataba
wa mwaka mmoja na Simba, Kisiga alisema hajarejea klabuni hapo kama
jina tu bali kwa ajili ya kuifanyia mambo klabu hiyo ya Msimbazi lakini
kikubwa anaomba ushirikiano.
“Ni kweli nimeshamalizana na Simba, kikubwa
ninachoweza kusema, halijarudi jina Simba bali nimerudi nikiwa
nimejipanga kwa ajili ya kufanya kazi kuona klabu inafanya vizuri kwenye
ligi na michuano mingine tutakayoshiriki,” alisema Kisiga ambaye msimu
uliopita aliichezea Mtibwa kwa mafanikio.
“Nina hamu, nina majukumu mazito kuhakikisha
nafanya kazi niliyokusudia, hivyo mashabiki wa Simba wasiwe na wasiwasi.
Kikubwa ni ushirikiano kwa wachezaji wenzangu na viongozi.”
Kisiga amesajiliwa baada ya kumaliza mkataba na
Mtibwa na mtu aliye karibu naye amedokeza kuwa ameweka kibindoni fedha
za usajili Sh5 milioni na atakuwa akipokea mshahara wa Sh1.5 milioni.
Wakati huohuo, jana Jumapili jioni, Mkenya
Kiongera aliyetoka KCB ya Kenya, alitarajiwa kusaini mkataba na Wekundu
wa Msimbazi hao na mambo yakienda vizuri, Elius Maguli na Mrundi Kwizera
nao watasaini.
0 comments :
Post a Comment