Familia
inayoundwa na wanandoa Bianca na Nick Bowser, ni familia yenye furaha
lakini iliyowashangaza wengi baada ya Nick ( baba wa familia) kupata
ujauzito na kujifungua.
Iko
hivi; Nick ambaye ana umri wa miaka 27 hivi sasa, alizaliwa na jinsia
ya kike na kupewa jina la Nicole na wazazi wake, lakini aliamua
kubadilika na kuishi kama mwanaume (transgender/jike dume) tangu miaka
saba iliyopita. Na hii ilichangiwa pia na sura na umbo la kiume
alilokuwa nalo.
Hali ilikuwa hivyo pia kwa Bianca
ambaye ana umri wa miaka 32 hivi sasa, yeye alizaliwa mwanaume na kuitwa
jina la Jason, lakini kutokana na kuwa na sura nzuri na umbo la kike,
na hisia zake za kutaka kuishi kama mwanamke, alibadili aina ya maisha
na kuishi kama mwanamke kamili.
Wawili hao walikutana na kuamua
kufunga ndoa huku wakiyabadilisha kabisa maisha ya wana ndoa, Nick akiwa
baba wa familia anaevaa na kuishi kama mwanaume. Mkewe Bianca (ambaye
ni mwanaume) yeye alibadili na kuishi kama mwanamke kamili akiihudumia
familia yake na kuvaa mavazi ya kike kama mama siku zote

0 comments :
Post a Comment