Wakati mwingine si kitu rahisi kupima ushawishi lakini tutaangalia ni
wazo mawazo gani ya mtu, mifano gani ya mtu, kipaji gani cha mtu na
ugunduzi gani wa mtu uliobadilisha jambo katika nchi yetu. Hawa ndio
mastaa 20 wa burudani, michezo na urembo Tanzania wenye ushawishi mkubwa
zaidi
1. Wema Sepetu

Well, well, well kunaweza kukawa na mjadala mrefu sana hapa wa kwanini
mrembo huyu akamate nafasi ya kwanza wakati kila kukicha amekuwa
akigonga vichwa vya habari kwa scandals kibao. Hiyo ni kweli lakini ukiugeuza umaarufu huo wa Wema na kuupeleka katika muktadha wa biashara na jinsi anavyokubalika,hakuna
anayemfikia Wema. Wema ni brand inayouzika kirahisi. Kuandikwa mara kwa
mara kwenye magazeti ya udaku ambapo mara nyingi si kwa kupenda yeye,
kumemfanya Wema awe dhahabu inayotamaniwa kushikwa na kila mtu. Habari
za Wema hapa Bongo5 zimekuwa zikipata hits (kusomwa zaidi) kuliko habari
yoyote ya staa yoyote yule unayemjua hapa Tanzania.
Iwe picha akiwa kwa daktari aking’olewa jino, picha za mtindo mpya wa
nywele, tattoo aliyojichora, picha za mbwa wake, Gucci na Vanny, picha
zinamuonesha akiwa na shoga zake Kajala na wengine, kila kitu kuhusu
Wema kinavutia attention ya watu. Story za Wema husomwa zaidi na kupata
comments nyingi kuliko za wengine wote.
Kama leo hii Wema akisema aanzishe bidhaa yoyote inayowalenga vijana,
haitachukua muda kushika na kutafutwa kama njugu. Wema ni show stopper!
Kama akiingia ukumbini kwenye shughuli, shughuli hiyo husimama kwa muda
kutokana na watu kugeuka kutaka kumwangalia kwa uzuri zaidi wakati
akielekea sehemu ya kukaa. Kutoka kuwa Miss Tanzania na sasa akiwa
muigizaji wa orodha A Tanzania, CEO wa kampuni ya filamu, Endless Fame
Films, Wema Sepetu ni mwanamke mwenye ushawishi mkubwa.
2. Diamond

Ni msanii gani Tanzania ambaye nyimbo zake zinahit mtaani bila hata
kupigwa redioni? Bila shaka umeshasikia nyimbo nyingi za Diamond mtaani
siku za hivi karibuni ukiwemo UKIMWONA na ukajiuliza iweje unahit wakati
haujaachiwa rasmi? Muziki wa Diamond umekuwa ukitumika kama tulizo la
wanyonge walio kwenye mahaba mazito. Kuanzia Mbagala,
Nitarejea, Lala Salama, Mawazo ama Nataka Kulewa, zote zimekuwa
zikitumiwa na watu wa rika mbalimbali, madaraja tofauti ya kiuchumi,
wanawake kwa wanaume na watoto kama burudisho la roho zao. Diamond
Platnumz hi hitmaker na haoneshi dalili za kupunguza kasi.
Diamond ndiye msanii anayefanya show nyingi zaidi ndani na nje ya
Tanzania na kwa kulipwa gharama kubwa kuliko msanii mwingine yeyote muda
huu. Hujaza kumbi kubwa za starehe yeye mwenyewe bila backup ya msanii
mwingine na kuwaacha wasichana wakibubujikwa na machozi ya furaha na
kutamani walau kukishika tu kifua chake kilichoanza kupasuka kwa
mazoezi.
Kwa mujibu wa kampuni ya Push Mobile, Diamond ambaye jina lake halisi ni
Nasib ndiye msanii anayeuza zaidi nyimbo zake kama miito ya simu (RBT).
Pamoja na kuzungukwa na scandal kibao kuhusu wanawake, Diamond ni kijana
mwenye mawazo pevu na ya kiutuuzima. Akiwa ametoka kwenye familia duni
na kupata misukosuko mingi ikiwemo kutengwa na baba yake na kulelewa
zaidi na mama yake, Diamond amekuwa akitoa ushauri na kuwapa moyo
watafutaji wa maisha wasikate tamaa. Hupenda kutoa ushauri kwa vijana
wenzie kuhusiana na umuhimu wa kujituma, kuchapa kazi, kumuabudu
mwenyezi Mungu na kutokata tamaa.
Katika kuhakikisha kuwa anaitolea pia jamii, hivi karibuni alitangaza
kuwa na nia ya kujenga msikiti. Ni kwa sababu zipi kijana huyu asiwe na
ushawishi?
3. Millard Ayo

Japo si kituo chake cha kwanza kuanza kazi, jina la Millard lilianza
kufahamika nchini kupitia kipindi cha Milazo 101 cha Radio One. Sauti
yake yenye mamlaka na ubunifu hewani, ulikifanya kipindi hicho kuwa
maarufu kuliko vingine vya burudani katika radio hiyo inayomilikiwa na
kampuni ya IPP.
Kuondoka kwake Radio One kulikuwa ni pigo kubwa lakini lenye neema kwa
Clouds FM. Alihamia Clouds FM na kuanzisha kipindi kipya kiitwacho
Amplifanya ambacho kilichukua nafasi ya kipindi cha nyimbo za kiafrika,
Bambataa. Haikuchukua muda kipindi cha Amplifanya kikawa miongoni mwa
vipindi bora kabisa Clouds FM.
Leo hii Millard ni miongoni mwa watangazaji bora Tanzania na
wanaosikilizwa zaidi. Si maarufu tu redioni bali pia ndiye mtangazaji wa
Tanzania mwenye mashabiki wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Ana
zaidi ya followers 40,000 kwenye Twitter huku Facebook akiwa na likes
zaidi ya 90,000.
Umaarufu wake kwenye mitandao ya kijamii umemfanya ageuke brand na
kuyavutia makampuni makubwa kama CRDB Bank, Fast Jet na mengine
kudhamini kile anachotweet. Tweets zake tu zinamuingizia fedha huku
akimiliki pia website yake binafsi yenye wasomaji lukuki. Pamoja na
kupata mafanikio hayo, Millard ameendelea kuwa mchapakazi, simple, mtu
anayejituma kutafuta habari hata sehemu za mbali kabisa, mcheshi na mtu
wa watu.
4. Nancy Sumari

Nancy Sumari ni msichana mrembo, mpole na mcheshi. Ndiye Miss Tanzania
wa kwanza aliyewahi kufika mbali zaidi kwenye shindano la Miss World
ambapo mwaka 2005 alifanikiwa kuwa Miss World Africa.
Kwa sasa Nancy ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kike, ni mwanafunzi
katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anasoma Shahada ya Biashara. Pia
ni mjasiriamali na anafanya kazi zake na jamii zikiwemo kuwahamasisha
watoto wa kike kujitambua na kuthubutu, ili kutimiza ndoto zao.
Katika harakati zake za kuhakikisha wasichana wa Tanzania wanatambua
haki zao, anaendesha programu iitwayo Mentorship, ambayo inazunguka
kwenye shule mbalimbali za serikali za wasichana nchini, na kuzungumza
nao kuhusu maisha. “Kwenye programu hiyo, tunabadilishana mawazo na
wanafunzi na wao wanazungumza changamoto wanazokutana nazo na kupeana
mawazo jinsi ya kufanya kwani nawaambia wakiamua kuthubutu wanaweza
kufanikiwa, na wanaonesha wanaweza,”Nancy aliliambia gazeti la Habari
Leo hivi karibuni.
Pamoja na hayo pia Nancy anashirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania
(TEA), kwenye kampeni ya kujenga mabweni ya wasichana kwenye shule za
sekondari za serikali nchini, ili kuhakikisha watoto wa kike wanapata
elimu.
Hivi karibuni alizindua kitabu chake kwaajili ya watoto ‘Nyota Yako’
kinachomlenga mtoto wa kike kuona jinsi wanawake wengine walivyofanikiwa
licha ya kupitia changamoto mbalimbali.
“Ninaamini kitabu kitasomwa na wengi ndio maana nikaamua ujumbe wangu
niufikishe kwa njia hii, watasoma watoto wetu hata wajukuu kitajenga
kitu kwenye akili ya mtoto na wakisoma shuhuda za hao waliofanikiwa nao
watathubutu” aliliambia Habari Leo. Tanzania itegemee mengi makubwa
kutoka kwa mrembo huyu.
5. Ambwene Yesaya aka AY

Safari ya AY mpaka kuja kuwa nyota anayefahamika Afrika nzima na sehemu
zingine duniani haikuwa rahisi. Amepitia mengi. Aliwahi kusema kuwa
kabla ya kufahamika Afrika Mashariki, alikuwa akienda Kampala na Nairobi
kufanya show za bure ili tu kukuza jina lake, jitihada ambazo zilizaa
matunda.
AY ni msanii smart, mbunifu, risk taker na anayeijua biashara ya muziki.
Ni msanii wa Tanzania anayefanya video za ghali zaidi ambapo mpaka sasa
video zake tatu, Speak With Your Body aliowashirikisha wamarekani Lamyia
Good na Romeo, Partyzone na Money zilimgharimu zaidi ya dola 70,000 kwa
pamoja kuzikamilisha. Video zake zimekuwa zikichezwa kwenye vituo
vikubwa vya runinga duniani.
Mwaka jana alifanikiwa kuandika historia kwa kushinda tuzo za Channel O
katika kipengele cha video bora ya mwaka ya Afrika Mashariki kwa wimbo
wake I don’t Wanna Be Alone aliowashirikisha Sauti Sol wa Kenya.
Umaarufu na busara zake ziliivutia kampuni ya simu ya Airtel mwaka jana
na kumteua kuwa balozi wake. Kwa sasa ni mwenyekiti mtendaji wa kampuni
ya burudani, Unity Entertainment, anajihusisha na biashara za nguo,
mwanzilishi wa kipindi cha televisheni cha Mkasi na biashara zingine.
Akiwa na followers zaidi ya 40,000 kwenye Twitter, mwaka huu AY amekuwa
msanii wa kwanza wa Tanzania kupata alama ya tick ya blue ya
verification kwenye mtandao huo. Ni watu watano tu nchini wana alama
hiyo.
6. Hasheem Thabeet

Hasheem Thabeet ni mtanzania wa kwanza kucheza kwenye ligi ya mpira wa
kikapu wa kulipwa nchini Marekani, NBA. Akiwa na urefu wa 7 ft 3 Hasheem
ndiye mchezaji mrefu zaidi kwenye ligi hiyo. Anacheza timu ya Oklahoma
City Thunder kwa mshahara wa dola milioni 5.128 kwa mwaka.
Pamoja na kuwa Marekani muda mwingi, Hasheem hasahau ya nyumbani na
hupenda sana kuongelea wasanii wa Bongo Flava kama alivyoandika.
“Mwaka 2000 mpaka mwaka 2005 Juma Nature alikuwemo katika kila nyimbo
ambayo ilikuwa hit ndani ya bongo. kubali au kataa. #fact.”
Akitumia Twitter, Hasheem anajulikana kwa jinsi anavyopenda kuandika
ujumbe wa matumaini. Hizi ni tweets 5 zenye ujumbe utiao matumaini
alizoandika hivi karibuni.
No matter what u go thru in life there is no need of gettin angry with
god and reflect bitterness to people around u. #havefaith.
The wise ones speak b’se they have something to say… fools speaks b’se
they have to say somethin. thik before u speak. #liveandlearn.
Everything can change in a blink of an eye… but dont worry; god never blinks. #believe #havefaith
Life aint about how hard u can hit… it’s about how hard u can get hit and still move forward.
Envy is a waste of time… accept what you already have, not what u need.
7. Flaviana Matata

Flavy ni mwanamitindo wa kimataifa aliyehamishia makazi yake nchini
Marekani. Amefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika fani hiyo kwa kushiriki
kwenye fashion show kubwa dunia, kufanya matangazo ya brand kubwa pamoja
na kuhusishwa kwenye majarida ya kimataifa.
Hivi karibuni Matata alishiriki katika kampeni za matangazo makubwa ya makampuni ya nguo ya DIESELna EDUN.
Kampeni ya DIESEL + EDUN ilianzishwa mwaka jana mwezi wa kwanza ambapo
muanzilishi wa kampuni ya DIESEL – Renzo Rosso – na waanzalishi wa
kampuni ya EDUN – Ali Hewson na Bono walisafiri hadi nchi za Uganda na
Mali na kukutana na wakulima wa pamba barani Africa.
Waliingia makubaliano ya kutengeneza nguo maalum zitakazotokana na pamba
ya wakulima hawa wa Afrika na hivyo kuwanufaisha moja kwa moja. Hivyo
basi nguo hizi zinatangazwa kama kampeni ili kunufaisha bara la Afrika.
Nguo hizo zitaanza kupatikana mwanzoni mwa mwezi wa tatu katika maduka
mbalimbali nchini Marekani na duniani. Pia nguo za DIESEL + EDUN
zitauzwa kupitia mitandao mbalimbali.
Flaviana ambaye aliwahi kuwa Miss Universe Tanzania 2007 anabaki kuwa
mwanamitindo pekee kutoka bara la Africa katika kushiriki katika kampeni
za nguo hizo.
Alianzisha taasisi ya Flaviana Matata Foundation inayohusika kuwasaidia
wasichana kupata karo ya shule, sare na mahitaji mengine muhimu. Pia
hutoa mafunzo na misaada kwa wanawake ili waanzishe miradi mbalimbali
ili kujiongezea kipato.
8. Loveness Diva

Diva Love Loveness ni mtangazaji maarufu zaidi wa vipindi vya usiku.
Ujasiri wake wa kuzungumza masuala ya mapenzi bila kificho
umemtengenezea maisha ya pande mbili, kupendwa sana na kuchukukiwa sana.
Ana mashabiki wengi.
Mara kadhaa kauli zake zimewahi kuleta mijadala mizito nchini lakini
bado kipindi chake cha Ala za Roho cha Clouds FM kimeendelea kuwa
kipindi chenye wasikilizaji wengi zaidi ukilinganisha na vipindi vingine
vya aina hiyo katika vituo mbalimbali vya radio nchini.
Diva pia hujihusisha na shughuli za kusaidia wasiojiweza kupitia mradi wake wa Diva Giving for Charity.
9. Masanja Mkandamizaji

Huenda watu wengi wanaweza wakawa hawafahamu kwamba Masanja ndiye staa
wa Tanzania mwenye likes nyingi Facebook, 104,670 na zaidi. Masanja ni
miongoni mwa wachekeshaji wa kizazi kipya wenye mashabiki wengi zaidi.
Umaarufu wake umetokana na kipindi cha Ze Komedi kilichoanzisha EATV na
sasa kikiwa TBC 1. Pamoja na kuwa mchekeshaji, Masanja ni muimbaji wa
nyimbo za injili, mchungaji mtarajiwa na mambo mengine. Huzitumia
akaunti zake za mitandao ya kijamii kuchekesha na kuwafurahisha zaidi
followers wake na ni miongini mwa mastaa wanaopata comments nyingi zaidi
kila wawekapo status.
10. Mwana FA

Hamis Corlone Mwinjuma aka Mwana FA ni rapper anayeaminika kuwa miongoni
mwa waandishi bora wa mashairi ya Hip Hop kuwahi kutokea katika muziki
wa kizazi kipya nchini Tanzania.
Jina lake lilianza kuvuma mwaka 1998 alipotoa ngoma yake ‘Ingekuwa
Vipi?’ akiwa na Jay Mo na pia ‘Mabinti’ ambayo ilitayarishwa na Bonny
Luv.
Mwaka 2003, ngoma yake ‘Alikufa Kwa Ngoma’ – ilimpa tuzo kama wimbo bora
wa Hip Hop wa mwaka kwenye Kili Music Awards. Mwana FA aliendeleza
utemi kwa kuachia hits kibao kama Unanitega, ‘Hawajui’ feat. Lady
Jaydee, Habari Ndio Hiyo akiwa AY, Bado Nipo Nipo, Unajijua Unanisikia,
Yalaiti na ngoma ya hivi karibuni Ameen.
Mwaka huu anasubiriwa kwa hamu kuachia ngoma yake mpya iitwayo Kama Zamani aliyowashirikisha Njenje.
Pamoja na kufanya muziki, Mwana FA aliamua kwenda nchini Uingereza
kuongeza shule yake ambako alisoma shahada ya Finance katika chuo kikuu
cha Coventry.
Ana mipango pia ya kuendelea na masomo ya PhD siku za usoni. Kwa sasa
ameanzisha pia kampuni ya kusimamia wasanii iitwayo Lifeline Music Inc
ambayo tayari ina msanii mmoja aitwaye Maua Sama.
11. Salama Jabir

Salama ni mhasisi wa kipindi cha Planet Bongo cha EATV ambacho enzi
anakifanya kilichangia ubora wa video za muziki wa Bongo Flava nchini
kutokana na kasumba yake ya kuzikosoa bila woga. Baada ya kuondoka EATV
na East Africa Radio, Salama alienda kusoma nchini Uingereza na kurudi
kukaa nje kwa muda na mambo ya habari. Alikuja kurejea tena na kipindi
cha Mkasi kinachorushwa EATV na kukifanya kuwa kipindi bora kabisa cha
mahojiano nchini. Salama ni mcheshi, mtundu na anaufahamu mkubwa wa
masuala ya burudani. Namna ya uulizaji wake wa maswali hufanya vipindi
vyake kuwa na mvuto zaidi.
12. Fid Q

Fareed Kubanda si rapper anayeheshimika tu kama mwandishi mkali wa
mashairi, bali pia anatambulika kwa kujihusisha kwake na shughuli za
kijamii.
January mwaka huu, Taasisi ya Under The Same Sun inayojihusisha na
kutetea haki ya watu wenye ulemavu wa ngozi, albino nchini, ilimtunuku
‘cheti cha shukrani’ kwa mchango wake katika kampeni ya shirika hilo.
Alipata cheti hicho baada ya mwaka jana kujumuika na taasisi hiyo katika
ziara yao ya kanda ya ziwa akiwa kama muelimishaji kwenye vita dhidi ya
mauaji ya ALBINO.
“Kujituma kwenye uchapaji kazi na utaratibu wa kuwa na nidhamu kazini ni
moja kati ya vitu vilivyowafurahisha,” aliiambia Bongo5.
Pia mwaka jana Fid alikuwa akiendesha darasa la hip hop la hiari jijini Dar es Salaam.
Akielezea madhumuni yake, Fid alisema, “Kwa haraka haraka hip hop darasa
maudhui yake ni kuwafundisha vijana wawe na positive thinking na
attitude kwa jamii, yaani wawe na fikira zilizopo katika mstari ulio
sahihi na hata kitabia, kwahiyo tunawajenga hivyo kupitia muziki wa
hiphop.”
13. Lady Jaydee

Mpaka sasa Lady Jaydee ana albam tano na hivi mwezi ujao ataachia albam
ya sita aliyoipa jina NOTHING BUT THE TRUTH. Ndiye msanii wa kike
Tanzania anayeheshimika na mwenye mafanikio zaidi. Jaydee ni
mjasiriamali ambaye hutumia pia kipato anachokipata kwenye biashara zake
kusaidia watu wanaohitaji msaada hususan watoto yatima wanaolelewa
kwenye vituo maalum.
Mwaka huu Lady Jaydee ambaye ana likes zaidi ya 47,000 Facebook na
followers zaidi ya 22,000 Twitter, aliweka historia kwa kufanikisha
safari ya kuupanda mlima Kilimanjaro na kuwa msanii wa kwanza wa kike
nchini kufanya hivyo.
13. Jacob Stephen

Jacob maarufu kama JB, ni muigizaji ambaye wachambuzi wa filamu za
Tanzania wanadai kuwa msanii pekee wa kiume anayeweza kufikia mafanikio
ya marehemu Steven Kanumba. Ni muigizaji wa kiume anayependwa zaidi kwa
sasa na filamu zake zimekuwa kivutio kwa watu wengi wa kila rika. Ana
uzoefu wa zaidi ya miaka 14 kwenye sanaa ya uigizaji.
Kwa sasa anamiliki kampuni ya filamu iitwayo Jerusalem ambayo imesaidia
kuwaibua wasanii wengine akiwemo Rose Ndauka, Elizabeth Kiyumba ’Nikita’
na wengine.Pamoja na kuwa muigizaji pia JB ni mhubiri wa masuala ya
dini.
15. Jokate Mwegelo

Jokate ni mtangazaji wa TV (Channel 0), muigizaji wa filamu, mwanamuziki
na mjasiriamali. Umaarufu wake ulianza aliposhiriki shidano la Miss
Tanzania mwaka 2006 na kukamata nafasi ya pili na kupata ubalozi wa
Redd’s na gazeti la The Citizen.
Jokate amewahi pia kushinda tuzo za ZIFF kama muigizaji bora wa kike.
Pamoja na hivyo hujihusisha na muziki pia ambapo amewahi kushirikishwa
na AY kwenye wimbo Kings and Queens na hivi karibuni amesikika kwenye
wimbo wa Lucci, Water up.
Hivi karibuni alijiingiza kwenye biashara ya ubunifu wa mitindo kwa
kuanzisha kampuni na brand ya Kidoti ambayo hubuni nguo pamoja na
kutengeneza nywele za aina mbambali zinazopatikana nchini.
16. Vanessa Mdee

Vanessa ni mtangazaji mahiri wa MTV Base na Choice FM. Uwezo wake mkubwa
wa kutangaza, maarifa kuhusu burudani na mambo mengine vimemfanya awe
miongoni mwa watangazaji wa kike wakali zaidi barani Afrika na wenye
mashabiki lukuki.
Vanessa amefanikiwa pia kwenye muziki ambapoi alimake headline sana
aliposhirikishwa na Ommy Dimpoz kwenye Me and You iliyotoka mwishoni mwa
mwaka jana. Sauti tamu kwenye chorus hiyo iliwashtua wengi kwakuwa
alikuwa akijulikana kama mtangazaji tu.
January mwaka huu aliachia single yake ya kwanza Closer. Ngoma hiyo
ilipokelewa vizuri na mashabiki wa muziki na miongoni mwa nyimbo
zilizopata downloads nyingi zaidi mtandaoni. Na sasa ametajwa kuwania
tuzo za Kili kama msanii bora anayechipukia huku wimbo Me and You
alioshirikishwa na Ommy ukitajwa pia kwenye vipengele kibao.
Ashafanikiwa kushare stage moja na wasanii wa kimataifa wakiwemo Mi Casa
Music wa Afrika Kusini.
17. Rita Paulsen

Maadam Rita anafahamika zaidi Facebook kwa wafuasi wake zaidi ya 25,000
kama mwanamke mwenye ushauri muhimu kuhusu maisha. Ni mwanzilishi wa
shindano kubwa la kusaka vipaji vya kuimba nchini, Bongo Star Search
ambalo limefanikiwa kutoa vipaji vingi na kwa kuwazawadia washindi
vitita vya pesa. Ni mcheshi, mrembo na ambaye siku zote hupenda kuwapa
moyo hata wale ambao uwezo wao ni mdogo.
18. Profesa Jay

Profesa Jay ni miongoni mwa wasanii waliyoifanya Bongo Flava ipate
mafanikio. Akiwa na albam nne mpaka sasa, Machozi Jasho na Damu 2001,
Mapinduzi Halisi 2003, J.O.S.E.P.H 2006 na Aluta Continua 2007, Prof
amewahi kushinda zaidi ya tuzo 6 mbalimbali zikiwemo za Kili. Mpaka sasa
hits zake zikiwemo Bongo Dar es Salaam, Jina Langu, Zali la Mentali,
Nikusaidije na zingine zinaendelea kutoa burudani isiyo na kifani katika
masikio ya mashabiki wake.
19. Dj Fetty

Fetty aka Fetilicious ni Dj pekee wa kike wa Tanzania aliyefanikiwa hadi
mwaka jana kupata shavu la kwenda kupiga muziki kwenye jumba la Big
Brother Africa. Ni msichana mrembo, anayejiamini na machachari hewani
huku akiwa na fanbase ya nguvu. Ana likes zaidi ya 57,000 kwenye
Facebook na followers zaidi ya 25,000 kwenye Twitter. Pamoja na kuwa
mtangazaji wa kipindi pendwa cha XXL, Clouds FM, Fetty ni dj kwenye club
ya Ambassodors Lounge jijini Dar.
20. Mzee Majuto

Kwa wengi King Majuto ni mchekeshaji bora zaidi nchini kuliko
wachekeshaji wote. Ni comedian wa kuzaliwa ambaye sura yake tu huwavunja
mbavu watu. Filamu zake zinauzika zaidi huku akiwa na mashabiki kibao
katika nchi zingine za Afrika zinazozungumza Kiswahili. Umaarufu wake
umemfanya apate deals za kufanya matangazo mbalimbali yakiwemo ya Airtel
na Azam.
“Jina la King Majuto limeweza kuwa maarufu zaidi kwake, kutokana na kazi
yake ya uigizaji katika filamu za vichekesho, mafanikio yake katika
uigizaji yamefanya waigizaji chipukizi kutamani kumshirikisha msanii
huyo mkongwe na wengine kujifunza kupitia kwake. Wapo wasanii chipukizi
ambao wanatamani kufika kiwango alichofikia King Majuto, akitamba katika
fani kwa zaidi ya miongo mitatu sasa bila kuchuja wala kutetereka
0 comments :
Post a Comment